World Literature

Submitted by: Submitted by

Views: 469

Words: 1087

Pages: 5

Category: Other Topics

Date Submitted: 03/21/2011 10:13 PM

Report This Essay

Imani ni moja ya mihimili muhimu katika jamii. Kupitia imani, jamii huweza kuwa na amani na mpangilio pia kuweza kufwata sheria fulani ambazo pia wanaweza kuhukumiwa kupitia hizo. Imani mara nyingi uhusiana na dini na kumuabudu Mungu au miungu. Kwa kutumia tamthilia mbili, The Crucible na Antigone vilivyoandikwa na waandishi marufu A. Miller na Sophocles, nitazungumzia dhamira ya imani katika tamthiliya hizi mbili na kuangalia kwa undani zaidi. Kwenye tamthilia ya The Crucible, mwandishi anaongelea zaidi kuhusu vitendo vya uchawi wakati kwenye Antigone, mwandishi amesisitizia zaidi kwenye mambo ya kimiungu.

Tamthilia ya Antigone ilioandikwa na mwandishi mashuhuri Sophocles, inafafanua juu ya imani za kijadi na kikabila ambazo Antigone jaribosi wetu alizozibeba pale aliposhikilia kumzika kaka yake Polynices kwenda kinyume na sheria za Creon. Kutokana na ugumu na uwezo wake wakulazimisha jambo, anajijengea msimamo thabiti na mkali katika uwamuzi wake, hata kama dada yake Ismene alionyesha udhaifu katika sheria alizoziweka Creon. Antigone alikuwa na imani kwamba kutokana na aibu waliyoipata na familia yao kutoka kwa baba yao Oedipus alitumia hii imani kuificha aibu yao na kutokuikasirisha miungu zaidi na kujiwekea msimamo wakumzika Polynices. “...many griefs our father Oedipus handed down...I will bury him myself...do as you like, dishonour the laws the gods hold in honor”. (Sophocles: 59, 63). Sophocles anaonyesha umuhimu wa mazishi na kiburi cha mwanamke kutii amri kupitia Antigone. Matendo yake yalionekana kupingwa na Creon kwani tabia yake ilikuwa si ya kawaida kwa mwanamke kwa sababau mambo ya nje yalikuwa hayawahusu na ilileta wasiwasi mwingi kwani alikuwa anaingilia ulimwengu wa wanaume ambao wangeshugulika kwenye mazishi. Kutokana na imani ya Antigone, anajikuta mpweke aliyetengwa na wahusika wote katika tamthiliya hii kutokana na msimamo wake. Mfano wa mtu ambaye hakukubaliana na msimamo wake ni mdogo wake Ismene. “What? You’d bury him- when a law forbids...